Usimamizi wa klabu ya Manchester United umemtimua meneja Erik Ten Hag kufuatia msururu wa matokeo mabovu ambapo klabu hiyo ni ya 13 ligini na kukosa kushinda mechi katika Europa League.
Red Devils chini ya Ten Hag imezoa pointi 11 pekee kutokana na mechi 9 za ufunguzi ikiwemokipigo cha jana cha mabao 2-1 ugenini kwa Westham United .
Ruud van Nistelrooy,ambaye amekuwa msaidizi wa Ten Hag ameteulliwa kaimu kocha huku mkufunzi wa kudumu akitafutwa.
Ten Hag ambaye alitokea Ajax Amstederm ya Uholanzi, alitua Old Traford mwaka 2022 na baada ya kunyakua kombe la FA mwezi Mei mwaka huu aliongezewa mkataba wa mwaka mmoja.
United wamelazimika kuingia sokoni kumtafuta kocha wa sita wa kudumu tangu kung’atuka kwa Sir Alex Ferguson, aliyestaafu mwaka 2013.
Ten Hag aliye na umri wa miaka 54 aliwasaidia mashetani wekundu kumaliza katika nafasi ya tatu msimu wake wa kwanza mwaka 2022.