Ligi Kuu FKF kurejea kwa raundi ya 5 baada ya mapumziko

Dismas Otuke
1 Min Read

Ligi Kuu ya FKF itarejea kati ya leo na Jumapili kwa  mechi za mzunguko wa tano, kufuatia mapumziko ya mechi za kimataifa.

Mathare United ambao wangali wanasubiri ushindi wa kwanza watawaalika Bidco United ugani Dandora Ijumaa kuanzia saa tisa.

Kesho kutapigwa mechi tano na nne siku ya Jumapili.

Jumamosi,Sofapaka itakuwa ugenini Machakos dhidi ya Nairobi City Stars, nao Bandari wawe nyumbani Mombasa Sports Club dhidi ya Murang’a Seal.

Kenya Commercial Bank itawatumbuiza  Kakamega Homeboyz katika uchanjaa wa Sportpesa Arena,nao Shabana FC wazuru Awendo kushikana mashati na Mara Sugar FC,kisha Posta Rangers imalize udhia na mabingwa watetezi Gor Mahia uwanjani Machakos.

Jumapili Tusker FC watakuwa Machakos dhidi ya Talanta FC ,Ulinzi Stars iwe mwenyeji wa Police FC katika uwanja wa Kinoru, kisha Kariobangi Sharks ipimane ubabe na AFC Leopards.

Share This Article