Serikali ya Cameroon yapiga marufuku habari za afya ya Rais Biya

Dismas Otuke
1 Min Read

Serikali ya Cameroon imepiga marufuku vyombo vyote vya habari nchini humo kuchapisha au kuzungumzia habari za afya ya Rais Paul Biya, kufuatia uvumi kuwa alikuwa ameaga dunia.

Waziri wa Usalama wa ndani nchini Cameroon Paul Atanga Nji, amesema kuwa taarifa hizo zinahatarisha amani na umoja wa taifa hilo, akiapa kuwachukulia hatua watakaokiuka agizo hilo.

Biya aliye na umri wa miaka 91 amekuwa mamlakani kwa zaidi ya miongo minne na hajaonekana katika maeneo yoyote ya umma tangu tarehe 8 mwezi uliopita, alipotoka Beijing kuhudhuria kongamano la China Africa.

Maafisa kadhaa wa serikali wamepuuza habari zilizozagaa kuhusu hali mbaya ya afya ya Rais huyo, wakisema kuwa yuko kwenye ziara ya kibinafsi mjini Geneva, Uswizi.

Licha ya uvumi huo haijulikani ni lini Biya atarejea nyumbani kutoka ulaya.

Share This Article