Mvuvi auawa na kundi hasimu Ziwa Victoria

Tom Mathinji
1 Min Read
Mvuvi auawa ziwa Viktoria.

Mvuvi mwenye umri wa miaka 23 Jacob Odira, ameuawa kufuatia mzozo wa eneo la uvuvi katika Ziwa Victoria.

Odira alifariki karibu na ufuo wa Lela katika kaunti ya Homa Bay, baada ya kushambuliwa na kundi hasimu la wavuvi.

Kulingana na polisi, Odira alikuwa akitekeleza shughuli za uvuvi akiwa na wenzake wanne katika eneo linalopakana na kaunti ndogo ya Rachuonyo, wakati wa shambulizi hilo.

Kundi hilo lilishambuliwa na wavuvi kutoka maeneo ya Ndhuru, Kamwai na Sikri katika kaunti ndogo ya Mbita.

Wavamizi hao waliowasili wakitumia mashua mbili, walishambulia kundi la Odira kwa vifaa butu vikiwemo  mawe na chupa, na kusababisha Odira kuanguka ndani ya ziwa na kufariki.

Mwili wake bado haujapatikana.

Akithibitisha kisa hicho, kamanda wa polisi wa kaunti ya Homa Bay Hassan Barua alisema uchunguzi umeanzishwa ili kuwachukulia hatua wahusika.

TAGGED:
Share This Article