Tume ya huduma ya taifa ya polisi, imerejelea kujitolea kwake kuimarisha maslahi ya maafisa wa polisi, ikiwa ni pamoja na marupurupu, mchakato wa uhamisho na mazingira jumla ya kazi, kuhakikisha maafisa hao wanatekeleza majukumu yao ipasavyo.
Afisa mkuu mtendaji wa tume hiyo Peter Lelei, alisema hayo alipozuru kibanda cha huduma ya taifa ya polisi, katika maonyesho ya kimataifa ya kibiashara ya Nairobi.
Lelei alisisitiza kuwa kutekeleza maswala hayo ni muhimu, kwani kutaimarisha utoaji huduma kwa wananchi, na kuwezesha hduma hiyo kutimiza mahitaji ya jamii.
Afisa huyo alitoa changamoto kwa maafisa wa polisi kuwa wabunifu katika maeneo yao ya kazi, huku akiwashukuru kwa kuwahudumia vyema wananchi.
Aidha aliwahakikishia maafisa wa polisi kote nchini, kuwa tume hiyo itaendelea kuwashika mkono kutokana na kujitolea kwao katika utoaji huduma.