Waziri Ogamba: watakaobainika kuhusika mkasa wa Endarasha kuadhibiwa vikali

Dismas Otuke
1 Min Read

Serikali itawaadhibu vikali wale watakaopatikana kuhususika katika kusababisha mkasa wa moto wa shule ya Hillside Endarasha Academy katika kaunti ya Nyeri.

Akizungumza mapema Alhamisi kwenye ibada ya wanafunzi 21 waliofariki kwenye shule hiyo, Waziri wa Elimu Julius Ogamba aliahidi kufanywa kwa uchunguzi wa kina kuhusu chanzo cha moto huo, huku wale watakaopatikana kuhusiwa wakichukuliwa hatua kali.

Moto huo uliozuka tarehe 5 mwezi huu katika bweni la wavulana wa shule hiyo ulisababisha vifo vya wanafunzi 21.

Mazishi ya wanafunzi hao yalicheleweshwa kutokana na uchunguzi wa DCI na pia ule wa kutathmini msimbojeni au DNA ya wanafunzi hao na wazazi wao ili kubainisha miili.

Miili ya wanafunzi 9 inatarajiwa kuzikwa leo huku mingine 10 ikizikwa kesho Ijumaa na mingine miwili siku ya Jumamosi.

Share This Article