Serikali ya Kwale kuendelea kuwekeza kwenye miradi ya maji

Marion Bosire
1 Min Read

Gavana wa kaunti ya kwale Fatuma achani amesema kuwa serikali yake itaendelea kuekeza zaidi katika sekta ya maji kupitia uchimbaji wa visima na mabwawa katika kaunti ya Kwale ili kuona kuwa wakazi wanapata bidhaa ya maji kwa matumizi ya nyumbani na kilimo cha unyunyiziaji maji mashamba.

Kulingana na Achani kuekeza zaidi katika sekta ya maji kutapiga jeki juhudi za serikali yake kutatua changamoto za upatikanaji wa maji Katika maeneo kame ikiwemo Lungalunga, Samburu na Kinango

Kaunti ya Kwale tayari imekamilisha uchimbaji wa mabwawa 17 katika maeneo mbalimbali ndani ya Kaunti hio, ikiwemo bwawa la Mwakalanga lililoko Mwereni gatuzi dogo la Lungalunga, bwawa la Nyalani katika wadi ya Puma eneo bunge la Kinango, pamoja na bwawa la Silaloni lililoko eneo bunge la Samburu.

Aidha, Kaunti hio imewezesha uchimbaji wa visima zaidi ya 44 katika maeneo bunge ya Matuga na Msambweni, pamoja na Upanuzi wa mifumo ya mabomba ya maji kwa zaidi ya kilomita 576, hatua hii ikinufaisha zaidi ya familia 3,000 katika kaunti hiyo.

Share This Article