Mke wa mwanamuziki wa Nigeria Ilerioluwa Oladimeji Aloba ambaye wengi walimgfahamu kama Mohbad amemkumbuka anapoadhimisha mwaka mmoja tangu alipoaga dunia.
Wunmi alitumia mitandao ya kijamii ambapo alilalamika kwamba marehemu mumewe alimwacha kwenye kibaridi ulimwenguni yeye pamoja na mwanao kwa jina Liam.
“Tulikuwa na mipango mingi ya maisha pamoja. Inaumiza sana kujua kwamba ndoto zetu hazitatimia. Leo nimechagua kusherehekea na kutoa heshima kwa urithi wako.” aliandika Wunmi.
Mohbad aliaga dunia katika njia ya kutatanisha mwaka mmoja uliopita wengi wakiamini kwamba aliuawa.
Video zilisambazwa mitandaoni zikionyesha mwanamzuki huyo dakika za mwisho mwisho akilia na kutaja mtu ambaye anaamini alipanga na kutekeleza njama ya kumuua.
Inasemekana kwamba Mohbad alikuwa akiishi kwa hofu kubwa. Kwenye video hiyo anasikika akizungumza lugha yake ya kiasili huku akimtaja mwanamuziki mwenza Zinoleesky.
Anasema Zino ndiye alimsema na kwamba alipatiwa maji akanywa ndipo akaanza kuhisi vibaya.
Mazishi yake pia yaliharakishwa sana ilhali yeye sio wa dini ya kiisilamu ambapo mtu huzikwa siku ya kifo chake.Jeneza lake pia lilikuwa dogo kuliko mwili wake hali ambayo ililazimu wapinde shingo yake ili atoshee humo.