Watoto wawili walifariki Jumanne usiku baada ya moto kuteketeza nyumba yao eneo la Kinangop, kaunti ya Nyandarua.
Kulingana na taarifa ya polisi, moto huo ulizuka saa 7:50 usiku, watoto hao wakiwa ndani ya nyumba peke yako.
Mama yao ambaye ni muuguzi katika zahanati ya Heni, alikuwa ameenda dukani kununua maziwa na aliporejea alipata nyumba ikiteketea.
Watoto hao wenye umri wa miaka sita na nne mtawalia, walichomeka kiasi cha kutoweza kutambulika, licha ya juhudi za wazima moto kutoka Naivasha kujizatiti kuuzima moto huo.
Miili ya watoto hao ilipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Engineer, kusubiri upasuaji.
Uchunguzi umeanzishwa kubaini chanzo cha moto huo.