Rais William Ruto leo Jumanne anatarajiwa kumtangaza rasmi aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga, kuwa mwaniaji wa Kenya wa wadhifa wa mwenyekiti wa Tume ya Muungano wa Afrika AUC.
Marais watano kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki wanatarajiwa kuhudhuriwa hafla hiyo, itakayoandaliwa katika Ikulu ya Nairobi.
Waziri huyo mkuu wa zamani atakabiliana na Mohamoud Youssouf wa Djibouti Anil Gayan wa Mauritius na Richard Randriamandrato wa Madagascar, kuwania wadhifa huo.
Wadhifa wa mwenyeki wa Tume ya Muungano wa Afrika AUC, unatarajiwa kuwa wazi mwezi Februari mwakani, baada kukamilika kwa muhula wa mwenyekiti wa sasa Moussa Faki Mahamat ambaye ni raia wa Chad.
Akiongea pembezoni mwa mkutano wa kimataifa wa mawaziri huko Tokyo kuhusu ustawi wa mataifa ya afrika (TICAD-9), uliokamilika siku ya jumapili, waziri mwenye mamlaka makuu Musalia Mudavadi, alisema baada ya Rais Ruto kumtangaza rasmi Raila kuwa mgombeaji wa wadhifa huo, serikali itazindua kampeini kabambe kuhakikisha kuwa Kenya inanyakua wadhifa huo.