Mawaziri wateule 19, wataapishwa Alhamisi asubuhi katika Ikulu ya Nairobi, saa chache baada ya bunge la taifa kuidhinisha uteuzi wao.
Sherehe hiyo ya kuapishwa kwa mawaziri hao itaongozwa na Rais William Ruto.
Kamati ya bunge kuhusu uteuzi iliwaidhinisha mawaziri wateule 19 huku ikikatalia uteuzi wa Waziri mteule wa jinsia Stella Lang’at.
Mawaziri hao wateule ni pamoja: Prof. Kithure Kindiki (Usalama wa taifa) Deborah Barasa (Afya), Alice Wahome (Ardhi), Julius Ogamba (Elimu), Soipan Tuya (Ulinzi), Andrew Karanja (Kilimo), Aden Duale (Mazingira), Eric Muuga (Maji na usafi), Davis Chirchir (Uchukuzu na Barabara) na Margaret Ndung’u (Habari na Uchumi wa Dinitali ).
Wengine ni John Mbadi (Fedha), Salim Mvurya (Biashara), Rebecca Miano (Utalii), Opiyo Wandayi (Nishati), Kipchumba Murkomen (Michezo), Ali Hassan Joho (Madini na Uchumi wa Baharini), Alfred Mutua (Leba), Wycliffe Oparanya (Vyama vya ushirika) na Justin Muturi (Utumishi wa Umma).