Benki Kuu yafanya mabadiliko katika sarafu ya Kenya

Tom Mathinji
1 Min Read

Benki Kuu ya Kenya, imefanya mabadiliko kadhaa katika sarafu za noti ya shilingi 50, shilingi 100, 200, 500 na ile ya shilingi 1,000.

Kupitia kwa taarifa benki hiyo ilisema noti hizo mpya sasa zitakuwa na sahihi ya Gavana wa wa benki hiyo Dkt. Kamau Thugge na katibu katika wizara ya Fedha Dkt. Chris Kiptoo.

“Tunahitaji kuwa na noti mpya. Sababu ya kuanzisha mabadiliko hayo katika noti za shilingi 1,000, ni kwamba huenda kukawa na upungufu wa noti hizo kati ya mwezi Julai na Agosti,” ilisema taarifa hiyo.

Noti hizo mpya pia zitaonyesha mwaka wa kuchapishwa na zitakuwa alama za kiusalama ambapo rangi zitakuwa zikibadilika katika kila noti ya shilingi 50,100,200,500 na 1,000.

Hata hivyo taarifa hiyo ilisema noti zilizoko kwa sasa zitaendelea kuwa halali na zitatumika sambamba na noti hizo mpya.

 “Uchapishaji wa noti hizo utaanza na zile za shilingi 1,000, huku za viwango vingine zikichapishwa katika miezi inayofuata,” ilisema taarifa hiyo.

Share This Article