Baadhi ya viongozi wa chama cha UDA katika kaunti ya Busia wametoa sasa wanapendekeza aliyekuwa Waziri wa Michezo kupewa wadhifa serikalini.
Namwamba ni miongoni mwa mawaziri waliyopigwa kalamu katika uteuzi mpya wa mawaziri uliofanywa na Rais William Ruto siku chache zilizopita.
Wakizungumza mjini Busia, viongozi hao wakiongozwa na mwenyekiti wa UDA kaunti ya Busia Maurice Chetambe walisema kama njia ya kukiimairsha chama eneo la magharibi, eneo hilo linahitaji kupata nafasi zaidi za uongozi kwa vile limeiunga mkono serikali kwa muda mrefu.
Aidha, wamesema hawakuona makosa yoyote ya uchapaji kazi wa Namwamba katika Wizara ya Michezo.
Badala yake, walisifia miradi ambayo ilitekelezwa na Namwamba wakati akihudumu katika wizara hiyo.