Rebecca Miano sasa ameteuliwa kuwa Waziri mpya wa Utalii.
Wadhifa huo awali ulishikiliwa na Dkt. Alfred Mutua ambaye sasa ameteuliwa kuwa Waziri wa Leba.
Akitangaza orodha yake ya kwanza ya Baraza Jipya la Mawaziri wiki jana, Rais William Ruto alikuwa amemeteua Miano ambaye awali alihudumu kama Waziri wa Biashara kuwa Mwanasheria Mkuu.
Ikiwa hilo lingetimia, Miano angekuwa mwanamke wa kwanza kuwahi kuhudumu katika wadhifa huo nchini.
Hata hivyo, orodha ya kwanza ya mawaziri walioteuliwa ilipowasilishwa bungeni jana Jumanne, jina la Miano lililkosekana na kuibua mdahalo wa kipi kilichotokea kwa uteuzi wake.
Kuhamishiwa kwa Miano hadi Wizara ya Utalii kuna maana kuwa taifa hili linatarajia uteuzi wa Mwanasheria Mkuu.
Mwanasheria Mkuu wa zamani Justin Muturi aliondolewa kwenye wadhifa huo na isitoshe ameteuliwa kuwa Waziri mpya wa Utumishi wa Umma.