Maafisa wa EACC wamkamata afisa mkuu wa Usorovea kaunti ya Kericho

Tom Mathinji
1 Min Read
Afisa Mkuu wa Usorovea kaunti ya Kericho Ismail Kipngeno Koskei, akamatwa na maafisa wa EACC.

Maafisa wa tume ya kukabiliana na ufisadi hapa nchini,EACC, wamemkamata mkuu wa Usorovea wa ardhi kaunti ya Kericho Ismail Kipng’eno Koskei, kwa madai ya kushiriki ufisadi.

Koskei, alimakatwa na maafisa hao baada ya kuitisha hongo ya shilingi 200,000 kutoka kwa mtu aliyefika afisini mwake kutafuta huduma za usajili wa ardhi.

Ardhi ya mlalamishi huyo ambayo ilikuwa imesajiliwa kwa jina la marehemu mamake, ilikuwa imeunganishwa na ardhi ya soko la Brooke linalomilikiwa na baraza la kaunti ya Kipsigis.

Afisi ya usorovea wa ardhi ilikuwa imetenagisha ardhi hiyo kutoka soko la Brooke, lakini mshukiwa huyo alitaka apewe hongo ya shilingi 200,000 ili hatimiliki ya mlalamishi itolewe.

Koskei alinaswa akiwa afisni mwake mjini Kericho, baada ya kupokea shilingi 100,000 kama malipo ya awali, huku akisubiri shilingi zingine 100,000.

Alipelekwa hadi katika makao makuu ya tume ya EACC kanda ya South Rift alikoandikisha taarifa, na sasa anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Central mjini Nakuru.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *