Watoto wafariki kwenye mkasa wa moto Nyahururu

Marion Bosire
1 Min Read

Mtaa wa mabanda wa Maina karibu na mji wa Nyahururu umeghubikwa na majonzi kufuatia mkasa wa moto uliosababisha vifo vya watoto wawili Jumapili alasiri.

Wawili hao mmoja wa umri wa miaka 7 na mwingine wa miaka minne walikufia kwenye nyumba yao ambako walikuwa wamefungiwa na mama yao mzazi ambaye alikuwa amekwenda kazini.

Wakazi waliohojiwa na wanahabari, wakiongozwa na mwenyekiti wa nyumba kumi Macharia Kahwai walielezea kwamba moto ulianzia kwenye mojawapo ya nyumba za eneo hilo ambazo zimejengwa kwa mbao kutokana na kinachoshukiwa kuwa tatizo la stima.

Macharia alisema kwamba wakazi walijaribu kuvunja nyumba ya watoto hao ili kuwasaidia bila mafanikio.

Familia zaidi ya 10 zimeachwa bila makao kufuatia mkasa huo na kulingana na jamaa kwa jina Mugo Nyaga anasema huo ni mkasa wa kumi wa moto umetokea katika eneo hilo katika muda wa mwaka mmoja.

Wakazi wa eneo hilo sasa wanataka viongozi waliochaguliwa wa eneo hilo kutekeleza ahadi zao.

Miili ya watoto hao ilipelekwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya rufaa ya kaunti ya Nyahururu.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *