Kajwang’: Usajili wa wapiga kura unapaswa kufutiliwa mbali

Tom Mathinji
1 Min Read
Seneta wa HomaBay Moses Kajwang'.

Seneta wa Homabay Moses Kajwang’, amehoji kwanini wakenya husajiliwa kuwa wapiga kura kutekeleza haki yao ya kikatiba ya kuwachagua wawakilishi wao.

Huku akipinga zoezi la usajiliwa wapiga kura, Kajwang’ aliwahimiza Maseneta wenzake kuidhinisha kwamba, mtu anapopata kitambulisho cha taifa, moja kwa moja anakuwa mpiga kura.

“Kwanini unahitaji kadi ya kupiga kura, ilhali una kitambulisho cha taifa?,” aliuliza Kajwang’.

Seneta huyo alidai kuwa mchakato wa usajili wa wapiga kura, ni hatua ya kwanza ya wizi wa kura.

“Punde tu unakuwa raia wa taifa hili, unakuwa na haki ya kupiga kura,” alisema Kajwang’.

Kulingana na Kajwang’, zoezi la usajili wa wapiga kura ni ya gharama ya juu, na serikali inapaswa kutupilia mbali zoezi hilo iwapo linataka kupunguza matumizi.

Alisema fedha za kuwasajili wapiga kura, zinaweza tumika katika miradi mingine.

“Mara ya mwisho Kenya ilitekeleza zoezi la usajili wa wapiga kura, taifa hili lilitumia shingi bilioni saba,” alidokeza Kajwang’.

“Fedha hizo zinaweza tumiwa kuwashughulikia madaktari na walimu wa Sekondari ya Msingi,” aliongeza Seneta huyo.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *