Rekodi ya Dunia ya Jepchirchir yarasimishwa

Dismas Otuke
1 Min Read

Rekodi ya Dunia ya marathoni ya mbio za wanawake pekee ya saa 2 dakika 16 na sekunde 16, iliyoandikishwa na Peres Jepchirchir imerasimishwa na Shirikisho la Riadha Duniani.

Jepchirchir ambaye pia ni bingwa mtetezi wa Olimpiki aliweka rekodi hiyo katika makala ya mwaka huu ya London Marathon yaliyoandaliwa Aprili 21.

Mwanariadha huyo pia yuko kwenye timu ya Kenya ya mbio za marathoni iliyo kambini huko Iten kujiandaa kwa michezo ya Olimpiki.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *