Rais William Ruto amesema Afrika inapaswa kuunga mkono benki ya African Export–Import, Afrexim.
Amesema Kenya inashukuru kutokana na ushirikiano ambao imekuwa nao na benki hiyo, hasa usaidizi ambao umetolewa na benki hiyo kwa ajenda ya maendeleo ya nchi hii.
“Afreximbank ni taasisi yetu. Inaunga mkono maendeleo yetu, ufadhili na utekelezaji wa miradi iliyotambuliwa,” alisema Rais Ruto.
Alizungumza hayo leo Ijumaa alipokutana na Rais wa benki ya Afrexim Benedict Oramah na maafisa wengine wa benki hiyo katika Ikulu ya Nairobi.
Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo ni miongoni mwa waliokuwapo.
Nchini Kenya, benki ya Afrexim inafadili miradi kadhaa ya ukanda maalum wa kiuchumi kama vile Dongo Kundu katika kaunti ya Mombasa, Sagana katika kaunti ya Kirinyaga na Nasewa katika kaunti ya Busia.