Junior Starlets yafuzu kwa fainali za Kombe la Dunia

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Kenya kwa wasichana walio chini ya umri wa miaka 17 almaaufu Junior Starlets imejikatia tiketi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza, baada ya kuibandua Burundi jumla ya mabao 5-0 katika raundi ya nne.

Kenya ilisajili ushindi wa mabao mawili kwa sufuri katika mchuano wa marudio wa raundi ya nne uliosakatwa kiwarani Ulinzi Sports Complex Jumapili alasiri.

Marion Serenge na Valerie Nekesa walitikisa nyavu kunako dakika za 17 na 21 mtawalia.

Kenya inajiunga na mataifa mengine 15 yaliyofuzu kwa kipute hicho yakiwa: Brazil, Colombia, wenyeji Dominican Republic, Ecuador, England, Japani, Korea Kaskazini, Mexico, New Zealand, Nigeria, Poland, Uhispania, Marekani na Zambia.

Fainali hizo zitaandaliwa kati ya Oktoba 16 na Novemba 3 mwaka huu huku Junior Starlets ikiwa timu ya kwanza ya soka kutoka Kenya kuwahi kushiriki Kombe la Dunia.

 

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *