Wizara ya elimu imetengewa shilingi bilioni 656.6 katika makadirio ya matumizi ya pesa za serikali ya mwaka 2024/25.
Alipowasilisha makadirio hayo katika majrngo ya bunge Alhamisi alasiri, waziri wa fedha na mipango ya uchumi Prof. Njuguna Ndung’u aisema mgao huo unajumuisha shilingi bilioni 358.2 kwa tume ya kuwaajiri walimu TSC, shilingi bilioni 142.3 kwa elimu ya msingi, shilingi bilioni 128 kwa elimu ya juu na utafiti, huku shilingi bilioni 30.7 kwa taasisi za kiufundi.
Aidha shilingi bilioni 13.4 za mgao huo, zitatumika kuwaajiri walimu wa junior secondary (JSS) kwa masharti ya kudumu nazo shilingi bilioni 30.7 zikitengewa kufanikisha elimu ya junior secondary.
Waziri Ndung’u alitenga shilingi bilioni 61.9 kwa elimu ya shule ya upili bila malipo na shilingi bilioni 9.1 kufanikisha elimu ya msingi bila malipo.
Wakati huo huo waziri huyo ametenga shilingi bilioni 3.2 kwa miundo msingi katika shule za msingi na upili, shilingi bilioni 1 kwa ujenzi wa madarasa ya junior secondary na shilingi bilioni 2.3 kwa ujenzi wa taasisi za kiufund.