Achebi ajiunga na Hand of God Promotions akijiandaa kwa pigano

Dismas Otuke
2 Min Read

Bondia wa Kenya Martin Achebi atashuka ulingoni tarehe 22 mwezi huu, kuzichapa dhidi ya na Luca Finon wa Mauritius, katika pigano lisilo la kuwania mkanda nchini Mauritius.

Achebi aliye na umri wa miaka 23 atalenga ushindi wa sita mtawalia katika amali yake, baada ya kushinda mapigani matano kupitia knock out dhidi ya wapinzani kutoka Kenya.

Achebi ni miongoni mwa wanamasumbwi wa humu nchini ambao wamesajiliwa na kampuni ya Hand of God Promotions, ambayo ndiyo ya hivi punde kupewa leseni ya kuhudumu na tume ya ndondi za kulipwa nchini Kenya KPBC.

Achebi amesema lengo lake ni kuendeleza ushindi lakini akasisitiza haja ya maslahi ya mabondoa kuangaliwa vizuri.

Achebi amesema azma yake ni kutwaa taji ya dunia katika uzani wa welter.

Rais wa KPBC Reuben Ndolo amekariri kuwa watatashirikiana na mapromoter, kuinua hadhi ya ngumi za kulipwa nchini .

Ndolo ameitaka serikali kuwekeza katika mchezo wa ngumi na kuwapeleka mabondia na wakufunzi nje ya nchi, ili kupata ujuzi.

Ndolo amesikita baada ya kenya kukosa kufuzisha hata bondia mmoja katika historia kwa michezo ya Olimpiki, kuanzia mwezi ujao jijini Paris Ufaransa.

Afisa mkuu mtendaji wa Hands of God Promotions Victor Olingo amesema lengo lao kuu ni kuimarisha maslahi ya mabondia.

Olingo ameongeza kuwa iwapo ndondi ya kulipwa itapata mapromota wazuri ina uwezo wa kutoa ajira kwa vijana nchini.

Website |  + posts
Share This Article