Bingwa wa Dunia katika mbio za mita 800 Mary Moraa,bingwa wa Jumuiya ya Madola Ferdinand Omanyala na mshikilizi wa rekodi ya dunia ya mita 3,000 kuruka viunzi na maji Beatrice Chepkoech ni miongoni mwa Wakenya watakaotimka mkondo wa tano wa Dimaond League wa Pre Fontaine Classic Jumamosi usiku mjini Eugene Marekani.
Moraa atashiriki mita 800 wakishindana na bingwa dunia mwaka 2019 Halimah Nakaayi kutoka Uganda,Jeema Reekie na Keely Hodgkinson wa Uingereza na Wamarekani Hurta Sage,Keylin Whitney na Hakins Nia pamoja na Goule Natoya wa Jamaica.
Omanyala kwa upande wake atakuwa akishiriki Diamond league msimu huu kwa mara ya kwanza huku akitiana jasho na Christian Coleman na Brandon Hicklin.
Chepkoech atashiriki mita 3,000 kuruka viunzi na maji pamoja na Faith Cherotich na Jackline Chepkoech watakaomenyana na Winfred Yavi wa Bahrain.