Gor Mahia wahifadhi ubingwa wa Ligi Kuu msimu wa 2023-2024

Dismas Otuke
1 Min Read

Klabu ya Gor Mahia  imehifadhi ttaji ya Ligi Kuu ya Kenya kwa ikifikisha mataji  21 ya  Jumapili jioni, baada ya kuilaza Muhoroni Youth mabao matatu kwa nunge katika uwanja wa Sport Pesa kaunti ya  Kirinyaga.

Benson Omala,Boniface Odhiambo na Austine Odhiambo walicheka na nyavu mara moja kila mmoja katika ushindi huo maridhawa ambao unawapa K’ogalo kombe la 21 zikisalia mechi tatu msimu ukamilike.

Mchuano huo ulihudhuriwa na Waziri wa TEHAMA na uchumi wa kidijitali Eliud Owalo aliyeahidi kuisaidia klabu hiyo kwa maandalizi ya mechi za kombe la Ligi ya mabingwa.

Waziri wa TEHAMA Eliud Owalo akijiunga na mashabiki kusherehekea ubingwa wa Ligi Kuu

Gor wamezoa pointo 67 wakiofuatwa kwa umbali na Tusker FC kwa alama 56, huku Police FC ikikalia nafasi ya tatu kwa pointi 54.

The Green Army wanavojulikana walinyakua taji ya ligi kuu ya Kenya miaka ya 1968, 1974, 1976, 1979, 1983, 1984, 1985, 1987, 1990, 1991, 1993, 1995, 2013, 2014, 2015, 2017, 2018, 2018–19, 2019–20, 2022-23 na 2023-2024.

Kufuatia ubingwa huo Gor Mahia wataiwakilisha Kenya katika mashindano ya kombe la Ligi ya mabingwa Afrika msimu ujao.

Share This Article