Rais Ruto ajadiliana na mwenzake wa Somalia katika Ikulu ya Nairobi

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais Ruto ajadiliana na mwenzake wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud.

Rais William Ruto leo Alhamisi ameshauriana na Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud katika Ikulu ya Nairobi.

Katika mkutano huo, Rais Ruto alielezea kujitolea kwa Kenya kushirikiana na Somalia katika kuimarisha amani na usalama katika kanda hii.

“Kenya imejitolea kufanya kazi na Somalia kuhakikisha kuna amani na usalama kanda hii,” ilisema taarifa katika ukurasa wa ikulu wa X.

Viongozi hao wawili walijadiiana kuhusu mbinu za kukabiliana na ugaidi na utovu wa usalama katika kanda hii.

Kenya na Somalia zinakabiliwa na changamoto za kiusalama kutoka kwa kundi la kigaidi la Al Shabab, ambalo mara kwa mara husababisha mashambulizi katika mataifa hayo mawili.

Share This Article