Alves aachiliwa huru baada ya kuwa jela miezi 14

Dismas Otuke
0 Min Read

Beki wa Brazil Dani Alves ameachiliwa huru kutoka gerezani nchini Uhispania baada ya kutumikia kifungo cha miezi 14.

Alves aliachiliwa Jumanne baada ya kulipa dhamana ya yuro laki moja unusu zilizohitajika na mahakama hiyo ya mji wa Barcelona.

Difenda huyo alikuwa amefungwa kufungo cha miaka minne unusu baada ya kupatikana na kosa la ubakaji.

Share This Article