Guinea itachuana na Mali katika mechi ya kuwania nafasi ya tatu na nne ya makala ya tatu ya mashindano ya kombe la Afrika kwa chipukizi walio chini umri wa miaka 23 nchini Morocco Ijumaa usiku uwanjani Ibn Batouta mjini Tangier.
Mali ilishindwa na wenyeji Morocco mabao 4-3 kupitia penati baada ya sare ya 2-2 katika nusu fainali, huku Guinea ikishindwa na mabingwa watetezi Misri bao moja kwa bila.
Mshindi wa nafasi ya tatu atajiunga na Morocco na Misri kushiriki michezo ya Olimpiki mwaka ujao jijini Paris Ufaransa.
Fainali ya kipute hicho itasakatwa Jumamosi katika uchanjaa wa Prince Mouley Abdelllah jijini Rabat kati ya Misri na Morocco.