Mohammed Salah alipachika penalti ya dakika za mwisho na kuinusuru Misri katika sare ya 2-2 dhidi ya Musumbiji katika mechi ya kwanza ya kundi B ya michauno ya AFCON.
Mchuano huo ulipigwa katika uwanja wa Felix Hoeffe Boigny jana Jumapili jioni huku Misri wakichukua uongozi kupitia kwa Mostafa Mohamed dakika ya pili.
Witi na Clesio Bauque walipachika magoli mawili ndani ya dakika tatu za kipindi cha pili na kuwaweka Mamba uongozini, kabla ya Mafarao kusawazisha kupitia penalti ya mwishoni mwa mechi.
Ilikuwa makala ya pili mtawalia kwa Misri ambao ni mabingwa mara saba wa kombe hilo kukosa kushinda mechi ya ufunguzi.