Agnes Jebet Ngetich avunja rekodi ya dunia ya kilomita 10 Valencia

Dismas Otuke
1 Min Read

Agnes Jebet Ngetich amevunja rekodi ya dunia ya kilomita 10 katika mbio za Valencia mpema Jumapili, akiweka rekodi mpya ya dakika 28 na sekunde 46.

Jebet aliye na umri wa miaka 22 amekuwa mwanamke wa kwanza kutimka mbio za kilomita 10 chini ya muda wa dakika 28.

Muda wa Jebet pia ni wa kasi kuliko rekodi ya dunia ya mbio za mita 10,000 inayoshikiliwa na Letesenbet Gidey ya dakika 29, sekunde 1.3.

Emmaculate Anyango pia amekimbia chini ya dakika 29 katika shindano la Jumapili akimaliza wa pili kwa dakika 28 na sekunde 57.

Mbio za wanaume zimeshindwa na Mganda Jacob Kiplimo aliyetumia dakika 26 na sekunde 48.

Share This Article