Jua na hali kavu kushuhudiwa maeneo mengi nchini Januari

Martin Mwanje
1 Min Read

Maeneo mengi ya nchi yatashuhudia jua na hali kavu angalau kufikia mwishoni mwa mwezi Januari mwaka huu. 

Hii ni kwa mujibu wa Mamlaka ya Utabiri wa Hali ya Hewa nchini.

Hata hivyo, mamlaka hiyo inasema eneo la Ziwa Victoria, Kusini mwa Bonde la Ufa, nyanda za chini za Kusini Mashariki mwa nchi, Nyanda za Juu Mashariki ya Bonde la Ufa na eneo la Pwani Kusini yatashuhudia mvua za hapa na pale.

Maeneo mengi ya nchi yameshuhudia mvua kubwa zilizonyesha katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.

Mvua hizo zilisababisha mafuriko katika baadhi ya maeneo huku kaunti 38 zikiathiriwa ikiwa ni pamoja Mombasa, Mandera na Wajir.

Serikali kuu, kupitia kwa kituo cha kamandi ya kitaifa ya kukabiliana na dharura na majanga ya mvua za El Nino, inasema jumla ya watu 174 walifariki kutokana na mafuriko hayo.

 

 

Website |  + posts
Share This Article