DCI yampongeza Omanyala kwa kutunukiwa tuzo ya MBS

Tom Mathinji
1 Min Read

Idara ya upelelezi wa jinai hapa nchini DCI, imempongeza mwanariadha Ferdinand Omanyala, baada ya kupewa tuzo ya Moran of the Order of the Burning Spear (MBS) na Rais William Ruto wakati wa sherehe ya 60 ya Jamhuri siku ya Jumatatu.

Mwanariadha huyo ambaye ni bingwa wa mbio za mita 100 za Jumuiya ya Madola mwaka 2023, ni afisa wa polisi wa idara ya DCI katika kitengo cha uchunguzi wa maabara.

Omanyala alikuwa miongoni mwa watu waliotuzwa katika hafla iliyoandaliwa katika Ikulu ya Rais, kutokana na michango yao ya kupigiwa mfano katika jamii.

Hivi majuzi Omanyala alituzwa na chuo Kikuu Cha Nairobi katika sherehe ya kumkaribisha nyumbani iliyoandaliwa katika ukumbi wa Chandaria.

“Omanyala, ambaye ni mwanariadha aliye na Kasi zaidi barani Afrika  na ambaye ameorodheshwa wa nane duniani, pia anasomea utaalam wa maabara katika maabara za DCI huku akisomea Somo la sayansi katika chuo Kikuu Cha Nairobi,” ilisema Idara ya DCI kupitia mtandao wa X.

Website |  + posts
Share This Article