Rais William Ruto ataongoza sherehe za kuadhimisha mwaka mmoja tangu kuzinduliwa kwa Hazina ya Hustler siku ya Alhamisi, katika kituo cha Green Park kaunti ya Nairobi.
Hazina hiyo ilikuwa miongoni mwa ruwaza ya Ruto kuwapiga jeki wafanyibashara wadogo.
Wateja milioni 21.2 wamejiandikisha kwa huduma hiyo ya mikopo kufikia sasa na jumla ya shilingi bilioni 36.8 zimetolewa.
Baadaye, serikali ilizundua Hazina ya Hustler kwa vikundi.