Vidosho wa Kenya Pipeline, KPC ndio mabingwa wa makala ya kwanza ya mashindano ya voliboli ya Afrika Mashariki ukanda wa tano.
Hii ni baada ya vidosho hao kuwazabua wenyeji Rwanda Revenue Authority, seti 3-0 katika fainali ya jana Jumapili jioni mjini Kigali.
KPC walisajili ushindi wa 25-20, 25-23 na 25-19 na kuandikisha historia ya kushinda mechi zao zote za mashindano hayo.