9 wafariki katika ajali ya barabarani Uasin Gishu

Dismas Otuke
1 Min Read

Watu tisa wameripotiwa kuaga dunia katika ajali ya barabarani iliyotokea mapema leo Ijumaa katika eneo la Soy, kaunti ya Uasin Gishu.

Ajali hiyo ilitokea majira ya saa moja asubuhi kwenye barabara ya Kitale-Eldoret ikihusisha lori na gari la abiria.

Kamanda wa polisi wa Uasin Gishu Benjamin Mwanthi, amesema kuwa dereva wa lori hilo alipoteza mwelekeo na kugoganga matatu hiyo iliyokuwa na abiria 12.

Watoto watatu pekee waliokuwa katika matatu hiyo ndio walionusurika kwenye ajali hiyo.

Matatu ilikuwa ikitoka Kitale ikielekea Eldoret wakati lori likielekea Kitale kutoka mjini Eldoret.

Ajali hiyo imetokea wakati ambapo makundi ya usalama wa barabarani yanaitaka serikali kutangaza ongezeko la ajali za barabarani nchini kuwa janga la kitaifa.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *