Maafisa wa usalama wameripoti kuwa takriban watu 60 wamefariki kutokana na shambulizi la kigaidi, lililotekelezwa katika jumba moja la kibiashara mapema Jumamosi.
Shambulizi hilo limetekelezwa katika jumba la Crocus City Hall viungani mwa Moscow, wakati wanaume kadhaa waliojifunika nyuso walipowafyatulia risasi raia .
Kulinga na shirika la usalama la Russia Federal Security Service (FSB), watu 40 walifariki papo hapo, huku wengine zaidi 100 wakijeruhiwa
Video iliyonaswa na Camera ilionyesha wanaume wanne wakiwashambulia watu waliokuwa wakiingia kuhudhuria tamasha la muziki chapa ya rock.
Yamkini baadhi ya washambuliaji hao walijifungia katika jumba la orofa ya juu ya jengo hilo, kulikosikika milio mingi ya risasi.
Polisi wanesema idadi hiyo ya waliofariki huenda ikapanda zaidi.
Milipuko kadhaa ilisikika huku sehemu ya jumba hilo ikiporomoka kufuatia makabiliano makali kati ya magaidi na pisi.
Polisi wangali wanaendesha msako kubaini adili ya magaidi hao.