Awamu inayofuata ya tamasha ya mzunguko ya miaka 30 ya Bongo Fleva nchini Tanzania itafanyika jijini Arusha.
Haya ni kulingana na tangazo lililotolewa na waandalizi wa tamasha hiyo kwenye akaunti rasmi ya Instagram, punde baada ya kukamilika kwa awamu ya Dodoma ya tamasha hiyo, Jumamosi Agosti 22, 2026.
Wakali wa awali wa muziki nchini Tanzania, watatumbuiza wakazi wa Arusha Septemba 12, 2026, lakini eneo la kuandaa tamasha bado halijawekwa wazi.
Katika taarifa hiyo, Hamadi Ally Seneda alishukuru wote waliofanikisha awamu zilizotangulia za tamasha hiyo wakiwemo wafadhili mbali mbali.
Alifafanua kwamba tamasha hiyo sio ya wanamuziki wakongwe kusherehekea urithi wao pekee, bali pia wameweka msingi wa kujenga upya na kuimarisha uchumi wa ubunifu nchini Tanzania.
Tamasha hiyo ya mzunguko ilizinduliwa kwa onyesho kubwa jijini Dar es Salaam Julai 10, 2026 kabla ya kuelekezwa Mwanza Agosti 8, kisha Dodoma Agosti 22 na sasa inasubiriwa awamu ya Arusha.
Waandalizi wamekuwa pia wakihusisha wasanii wa muda mrefu kutoka nchini Kenya.