2Baba amsherehekea mkewe Annie kwenye siku yake ya kuzaliwa

Marion Bosire
1 Min Read

Innocent Idibia mwanamuziki wa Nigeria, anayefahamika kama 2baba, ameonyesha mapenzi kwa mke wake Annie kupitia mitandao ya kijamii, alipokuwa akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

Annie Idibia ambaye ni mwigizaji wa filamu za Nollywood, alitimiza umri wa miaka 40 jana Novemba 13, 2024, na amekuwa akikumbusha wafuasi wake mitandaoni kuhusu siku hiyo muhimu.

Katika mojawapo ya machapisho yake mitandaoni, Annie alikiri kwamba hana kila kitu akitakacho maishani ila anaridhika alivyo.

Wafuasi wake hata hivyo walikuwa na wasiwasi baada yake kuchapisha video ya kufurahia ujio wa siku yake ya kuzaliwa ambapo hakuonekana mwenye furaha.

2Face alichapisha picha ya Annie kwenye akaunti yake ya Instagram na kuiambatananisha na wimbo maarufu mitandaoni wa kukiri mapenzi.

Ndoa ya wawili hao hata hivyo imekumbwa na matatizo awali kiasi cha Annie kutangaza mitandaoni kwamba mume wake sio mwaminifu.

Annie aliwahi kufichua kwamba alikutana na 2Baba kabla yake kupata mtoto na mwanamke yeyote na akafanya hivyo akiwa kwenye ndoa naye jambo alilosema lilimuumiza sana.

Alijitia moyo akisema kwamba mazuri ya ndoa yao ni mengi kuliko mabaya.

Share This Article