Idadi ndogo yashuhudiwa katika uwanja wa Kinoru kwenye usajili wa NYS

Marion Bosire
1 Min Read

Idadi ndogo ya vijana walijitokeza leo kwa usajili wa makurutu wa huduma ya vijana kwa taifa NYS katika uwanja wa michezo wa Kinoru katika kaunti ya Meru leo, ikilinganishwa na idadi inayoshuhudiwa wakati wa usajili wa polisi na jeshi.

Wengine kati ya wliojitokeza walikosa fursa hizo za usajili kutokana na kutoafiki gredi inayohitajika ya mtihani wa kidato cha nne KCSE.

Mojawapo ya masharti ya usajili ni mtu awe alipata alama ya D- kwenye mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne KCSE.

Wengine walifungiwa nje kwa kuchelewa kufika kwenye uwanja wa Kinoru huku binti mmoja akikosa fursa kwa kuwa na mchoro kwenye mkono wake wa kushoto.

Visa vya vyeti gushi vya masomo havikishuhudiwa kwenye usajili huo wa Meru ambao lengo lilikuwa kupata makurutu 16 kutoka kaunti ndogo ya Imenti Kaskazini.

Walioteuliwa watajiunga na wenzao kwa mafunzo katika taasisi ya NYS ya Gilgil katika kaunti ya Nakuru na baadaye kupokea mafunzo ya kiufunzi katika kozi mbali mbali.

Waliokosa fursa kutokana na gredi za chini walihimizwa kurejea shuleni kuziboresha au wajiunge na taasisi za mafunzo ya kiufundi.

Share This Article