Polisi siku ya Jumapili wamewakamata washukiwa 14 kwa kutekeza ,kuharibu na wizi wa mali ya mamilioni ya pesa ya mbunge wa Molo Kimani Kuria, wakati wa maandamano ya vijana wa Gen Z kupinga mswada wa fedha.
Polisi pia wamepata baadhi ya mali iliyoibwa ikiwemo ng’ombe wanne kati ya saba walioibwa kutoka kwa boma la mbunge huyo, ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya fedha na mipango katika bunge a kitaifa.
Mali nyingine iliyopatikana ni pamoja na vifaa vya umeme,blanketi,meza na viti.
Kuku 2000 waliteketezwa huku wengine takriban 8,000, wakiibwa na kundi hilo la waandamanaji ambalo pia liliharibu magari na kuvunja madirisha ya vioo vya nyumba .
Washukiwa hao watafikishwa mahakamani kwa kuiba ,kuharibu na kumiliki mali ya wizi ya mbunge huyo.
Ng’ombe walioibwa ni wa thamani ya shilingi 300,000 kila mmoja na mbuzi 29 wakati wa uvamizi huo.