Kampuni ya kutoa huduma za mawasiliano ya Safaricom PLC imetangaza ongezeko la mapato yake kwa asilimia 2 nukta 1 hadi shilingi bilioni 34 nukta 2 kwa kipindi cha miezi sita kilichokamilila Septemba mwaka 2023 kutoka kwa biashara yake mpya nchini Ethioipia.
Kampuni hiyo ilirekodi ukuaji wa asilimia 10 nukta 9 kwa biashara ya Kenya hadi shilingi bilioni 41 nukta 6 kwa kipindi cha nusu mwaka .
Safaricom imenakili ukuaji wa pato lake hadi shilingi bilioni 158 katika kipindi hicho ,kiwango kikubwa kutokana na M-Pesa na mauzo ya data.