Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, amemwondoa mamlakani Mkuu wa Majeshi ya Ukraine Oleksandr Syrskyi, baada ya siku kadhaa za maandamano kupinga kutimuliwa kwa Waziri wa Ulinzi Mykhailo Fedorov.
Nafasi ya Syrskyi mwenye umri wa miaka 60, imechukuliwa na Jenerali Mykhailo Drapatyi mwenye umri wa miaka 43, ambaye anajulikana kwa uzoefu wake mkubwa vitani na umaarufu miongoni mwa wanajeshi.
Baada ya kutekeleza mabadiliko hayo, Zelensky alimshukuru Syrskyi kwa kulinda Kyiv na kuongoza mashamabulizi yaliyosababisha ushindi dhidi ya adui.
Akichukua wadhifa huo, Drapatyi alisema atatekeleza wajibu wake kwa umakini na kuheshimu wale wote wanaolinda taifa hilo.
Waziri wa zamani wa Ulinzi Fedorov kupitia ujumbe kwa Telegram, alimpongeza Drapatyi akitaja uteuzi huo kuwa matumaini makubwa katika juhudi za kutafuta haki na uhuru.
Wakati huo huo alimshukuru Syrskyi kwa juhudi zake za kuilinda Ukraine.