Mazungumzo kati ya Xi Jinping na Vladimir Putin yamehitimishwa baada ya kudumu kwa zaidi ya saa mbili, huku Putin akiondoka katika makazi ya serikali ambako mkutano huo ulifanyika, kwa mujibu wa shirika la habari la serikali ya Urusi, TASS.
TASS imesema kuwa miongoni mwa ajenda zilizojadiliwa na ujumbe wa viongozi hao wawili ni “matarajio ya kuimarisha zaidi ushirikiano wa kiuchumi kati ya Urusi na China.”
Katika nukuu ya hotuba za ufunguzi za Xi na Putin, iliyochapishwa na Kremlin, viongozi hao wawili walisifu uhusiano wa nchi zao na kubainisha kuwa huu ulikuwa mkutano wao wa tatu wa ana kwa ana mwaka huu.
Xi alizihimiza nchi hizo mbili “kuendelea kusonga mbele kwa uthabiti na ujasiri, huku zikifungua daima uwezo mkubwa uliopo katika mahusiano ya pande mbili.”
Kwa upande wake, Putin alieleza ukuaji wa biashara kati ya nchi hizo mbili na kusisitiza kile alichokiita “mazungumzo yenye tija katika utafiti wa kisayansi na ubunifu.”
Taarifa ya BBC