Wenyeji Harambee Starlets ya Kenya watakabiliana na Australia kwenye fainali ya mechi za kirafiki za FIFA series Jumatano hii katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo.
Mchuano huo utaanza saa kumi na moja unusu jioni na utatanguliwa na ule wa kutafuta mshindi wa nafasi ya tatu na nne kati ya Malawi na India kuanzia saa nane adhuhuri.
Kenya iliwalemea India mabao 2-0 huku Australia maarufu kama Matilda wakiititiga Malawi mabao 5-0, katika mechi za ufunguzi Jumamosi iliyopita.
ni mara ya kwanza kwa Kenya kuandaa mechi hizo za FIFA series ambazo hutumika na timu kujiandaa.
Tiketi za mchuano wa Kenya na Australia zinauzwa kwa shilingi 100 kwa zile za kawaida,shilingi 1,000 kwa zile za jukwaa kuu na shlingi 5,000 kwa zile za VVIP.