Waziri wa Afya Aden Duale ,amesema kuwa zaidi ya hospitali za kibinafsi 1,000, nchini zimefungwa baada ya kujaribu kutapeli pesa za mamlaka ya Afya ya umma SHA.
Akizungumza Jumamosi Waziri Duale amefichua kuwa baadhi ya hospitali hizo zimo katika kaunti za Homa Bay,Bungoma,Mandera,Wajir na Kisii akisisitiza kuwa hsopitali zaidi ya 10 zimenaswa na kufungwa mwezi Machi pekee.
Aidha hospitali nyingine 250 zinachungwa na maafisa wa DCI,30 zikiwa zimefunguliwa mashataka huku nyingine 18 zikifikishwa kortini.
Alisema haya Jumamosi alipohudhuria mahafala ya kufuzu kwa wasichana waliokamilisha masomo ya dini ya Kiislamu katika kituo cha Hawa Kosar ambapo wasichjana 25 walihitimu.