Watu 40 wafariki kutokana na mafuriko Angola

Vifo zaidi vimeripotiwa katika mikoa ya Cuanza Sul na Malanje.

Tom Mathinji
1 Min Read
Watu 40 wafariki Angola kutokana na mafuriko.

Takriban watu 40 wamefariki nchini Angola kufuatia mvua kubwa, huku wengine kadha wakiwa hawajulikani waliko.

Kulingana na maafisa nchini humo,watu 13 wamefariki Jijini Luanda huku wengine watano wakiwa hawajulikani waliko, ilhali wengine 26 wakifariki na wengine wanne wakiwa hawajulikani waliko mjini Benguela kufikia Jumatano.

Vifo zaidi vimeripotiwa katika mikoa ya Cuanza Sul na Malanje.

Mafuriko makubwa mwishoni mwa wiki yaliharibu barabara na makazi katika jiji kuu Luanda, na mji wa pwani wa Benguela.

Zaidi ya nyumba 600 zimeharibiwa, na zaidi ya makazi 9,500 kujaa maji ya mafuriko na kuathiri zaidi ya watu 51,000.

Makundi ya dharura yanahusika katika kuondoa maji ya mafuriko na kutoa chakula na maji safi ya kunywa, huku maafisa wakisema hali inaendelea kuimarika.

TAGGED:
Share This Article