Watalii wanusurika kufuatia ajali ya meli Marekani

Takribani abiria na wafanyakazi 180 hadi 190 walikuwa ndani ya meli hiyo wakati ajali ilipotokea.

Tom Mathinji
1 Min Read
Meli ya kitalii yagongana na ile ya mafuta kwenye mto Mississipi nchini Marekani.

Watalii waliokuwa wakisafiri kutumia meli ya kifahari, wana sababu ya kutabasamu baada ya kunusurika ajali, meli yao ilipogongana na ile ya mafuta katika mto Mississipi, New Orleans, nchini Marekani.

Meli hiyo ya kitalii iliyokuwa imetia nanga kwenye mto huo ilipinduka na kuzama ndani ya maji muda mfupi baada ya ajali hiyo iliyowatia hofu wasafiri na waliokuwa karibu wakati wa ajali hiyo.

Akithibitisha ajali hiyo, Meya wa New Orleans, Helena Moreno, alisema watu wote waliokuwa ndani ya meli hiyo waliokolewa na kuhesabiwa, huku 32 kati yao wakipelekwa hospitalini kwa matibabu.

Wafanyakazi wa bandari, wazima moto na watu waliokuwa karibu na eneo la tukio hilo, walishirikiana kwa pamoja katika shughuli hizo za uokoaji.

Takribani abiria na wafanyakazi 180 hadi 190 walikuwa ndani ya meli hiyo wakati ajali ilipotokea.

Share This Article