Washukiwa wa mauaji ya mwanablogu wa Meru kufanyiwa uchunguzi wa akili

Tom Mathinji
1 Min Read
Washukiwa wa mauaji ya mwanablogu Daniel Muthiani.

Washukiwa wawili wanaohusishwa na mauaji ya mwanablogu wa Meru Daniel Muthiani almaarufu Sniper, watazuiliwa kwa siku saba zaidi, ili wafanyiowe uchunguzi wa kiakili.

Hatua hiyo inafuatia agizo lililotolewa na naibu msajili wa Mahakama kuu ya Kiambu Jackline Karani, alisema wawili hao wafanyiwe uchunguzi wa kiakili kubaini iwapo wanaweza kufunguliwa mashtaka.

Vincent Mureithi Kirimi almaarufu Supuu na Murangiri Kenneth Guantai almaarufu Tali,watazuiliwa katika kituo cha polisi cha Muthaiga hadi tarehe 29 mwezi Januari, watakapofikishwa mahakamani.

Awali afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma ilisema kuwa inaushahidi wa kutosha kuwafunguliwa mashtaka ya mauaji Vincent Mureithi Kirimi na Murangiri Kenneth Guantai, baada ya kufanya uchunguzi wa kina.

Mmoja wa washtakiwa hao ni nduguye Gavana wa Meru Kawira Mwangaza.

Mkurugenzi wa mashtaka ya umma pia amewasilisha kesi dhidi ya washukiwa wengine watano, inayoshughulikiwa katika mahakama ya Kibera.

Mwanablogu huyo wa Meru aliripotiwa kupotea tarehe mbili mwezi Disemba mwaka jana, huku mwili wake ukipatikana umetupwa katika mto Mutonga kaunti ya Tharaka Nithi tarehe 16 mwezi huo wa Disemba.

Share This Article