Waandalizi wa tamasha ya Roast and Rhyme Reggae Ragga Nyam Nyam edition wametoa orodha ya wasanii wanaotarajiwa kutumbuiza kwenye makala ya mwaka huu Machi 22, 2026.
Hafla hiyo itakuwa pia ya kusherehekea miaka 10 tangu kuanzishwa kwa tamasha hiyo, katika uwanja wa mchezo wa magongo wa Lugogo.
Awamu ya mwaka huu ya tamasha hiyo, itakuwa na wasanii nyota wa Uganda kama vile King Saha, Kapeke, Kalifah Aganaga na John Blaq.
Wasanii wengine watakaokuwepo ni Double Black, Ivuga Band na C Wayne, wakiandamana na wapiga muziki kadhaa ambao watahakikisha uendelevu katika tamasha hiyo.
kampuni ya muziki ya Swangz Avenue ndiyo huandaa tamasha ya Roast And Rhyme, tamasha ambao imekua hadi kiwango cha matamasha ya mitindo ya maisha ya watu wa Uganda.
Watakaohudhuria watafurahia muziki wa Uganda moja kwa moja, nyama ya kuchomwa, mitindo ya mavazi, michezo na mandhari ya eneo hilo.
Waandandilizi wa tamasha hiyo wameahidi mwonekano bora zaidi mwaka huu, ambapo jukwaa litakuwa bora na mifumo ya sauti, mwangaza na picha pia ikiboreshwa.
Malango ya tamasha hiyo yatafunguliwa saa tano asubuhi.