Wanyonyi na Chebet wahifadhi tuzo za SOYA

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa wa Dunia Emmanuel Wanyonyi na Beatrice Chebet, wametawazwa wanamichezo bora wa mwaka uliopita katika tuzo za kila mwaka za SOYA wakati wa hafla ya 22, iliyoandaliwa Ijumaa usiku katika  bustani ya Uhuru Gardens.

Ulikuwa mwaka wa pili mtawalia kwa Wanyonyi na Chebet kutawazwa washindi wa tuzo hizo baada ya kuibuka bora mwaka 2024 ambao tuzo zake ziliandaliwa mwaka jana.

Wanyonyi kando na kutawazwa bingwa wa Diamond League katika mita 800 ,alinyakua dhahabu ya dunia huku chebet akishinda dhahabu za Dunia mjini Tokyo,Japan katika mita 5,000, na 10,000.

Hafla hiyo ya kufana ilihudhuriwa na mshikilizi wa zamani wa rekodi ya Dunia katika mbio za Marathon Haile Gebrselassie kutoka Ethiopia.

Share This Article