Wanyonyi aibuka wa pili, Odira wa tatu, Rabat

Bingwa wa Dunia upande wa wanawake Lillian Odira alishiriki Diamond League kwa mara ya kwanza, akimaliza wa tatu kwa muda wa dakika 1 sekunde 57.27.

Dismas Otuke
1 Min Read

Bingwa wa Dunia na Olimpiki katika mbio za mita 800 Emmanuel Wanyonyi alimaliza katika nafasi ya pili katika mkondo wa tatu wa Diamond League ulioandaliwa Jumapili usiku katika uwanja wa Prince Moulay, jijini Rabat, Morocco.

Wanyonyi aliyekuwa akifungua msimu wa Diamond League, alitimka kwa dakika 1 sekunde 43.56, nyuma ya Mwingereza Max Burgin aliyeibuka mshindi kwa dakika 1 sekunde 42.98.

Bingwa wa Dunia upande wa wanawake Lillian Odira alishiriki Diamond League kwa mara ya kwanza, akimaliza wa tatu kwa muda wa dakika 1 sekunde 57.27.

Audrey Werro wa Uswizi alishinda mbio hizo kwa dakika 1 sekunde 56.56,akifuatwa na Tsigie Duguma wa Ethgiopia  kwa dakika 1 sekunde 57.24.

Simon Koech na Edmund Serem, walichukua nafasi za tatu na nne mtawalia katika mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na maji.

Mbio hizo zilishindwa na bingwa mara mbili wa Olimpiki Soufiane El Bakkali wa Morocco.

Share This Article